Official YouTube channel of Pastor, Ev.WILLIAM SIFUNI MCHOME. Subscribe for more Inspirational, Educational and Spiritual Warfare Videos .
Channel Rasmi ya YouTube ya Mchungaji, Mwnj. WILLIAM SIFUNI MCHOME.Jiunge nasi kwa kubofya Subscribe ili upate video za kiroho, za mafundisho, na za vita vya kiroho.

Vision: โ€œBring as many People as โ€œPossible to Our Almight GOD.
Maono: "Kuwaleta watu wengi iwezekanavyo kwa Mungu wetu Mwenyezi.

Mission: To Spread the Scripture of Our Almight GOD all the time through spiritual and diaconic services
Dhamira:"Kueneza Maandiko Matakatifu ya Mungu wetu kila wakati kupitia huduma za kiroho na za diakonia."

Luka 18:27
"Yasiyowezekana kwa wanadamu, yawezekana kwa Mungu."

Yanawezekana yote kwa YESU ukiamini tu

Unaweza kusimama na huduma hii kwa USHAURI na SADAKA yako.

+255656870833 {namba ya SADAKA na HUDUMA}

+255787493443 {Whatsapp namba ya Mtumishi W.S.MCHOME}


YAWEZEKANA Tv

SHALOM WAPENDWA KATIKA BWANA! ๐Ÿ™๐Ÿ”ฅ

Kwa neema ya Mungu, tunakualika kwenye IBADA YA OMEGA ALFA ya kipekee ya kumaliza mwezi na kuanza mwezi mpya katika uwepo wa Mungu.

๐Ÿ”ฅ MAOMBI NONSTOP MASAA 12

USIINGIE MWEZI WA 7 BILA MAOMBI!

Tutamaliza Mwezi wa 6 na Yesu na kuanza Mwezi wa 7 na Yesu, sambamba na Kutangaziwa Neno la Mwezi wa 7.

๐Ÿ—“ KUANZIA: Jumanne, 30/06/2026
๐Ÿ• Saa 1:00 Usiku

๐Ÿ—“ MPAKA: Jumatano, 01/07/2026
๐Ÿ•› Saa 12:00 Alfajiri

๐Ÿ“บ LIVE kupitia YAWEZEKANA TV โ€“ YouTube

Nakuomba usikose. Mwalike na mwingine ili kwa pamoja tuumalize mwezi katika maombi na tuuanze mwezi mpya tukiwa mbele za Mungu. Ninaamini Bwana atatenda jambo jipya katika maisha yako.

Karibu sana. Mungu akubariki! ๐Ÿ™๐Ÿ”ฅ

8 hours ago | [YT] | 0

YAWEZEKANA Tv

Usikose tukeshe tukiomba kinyume na roho za mauti na uharibifu

1 week ago | [YT] | 14

YAWEZEKANA Tv

Day 2/90


*Siku ya Pili - Neema ya Kuzaa na Kukata Utasa Kwenye Kila Eneo la Maisha Yako*:

UTASA ni Hali ya KIROHO inayofanya usizae Matokeo

*MAANDIKO YA KUSOMA*
Wapendwa Shika na usome haya kwa imani kabla na baada ya maombi:
1. *Mwanzo 30:22* - "Mungu akamkumbuka Raheli, akamsikia, akamfungua tumbo lake."
2. *Kutoka 23:26* - "Hakutakuwa na mwanamke mzaa mimba wala tasa katika nchi yako; nitaitimiza hesabu ya siku zako."
3. *Zaburi 113:9* - "Humfanya yule tasa akae nyumbani, awe mama afurahiye watoto. Haleluya!"
4. *Isaya 54:1* - "Piga kelele kwa furaha, wewe tasa usiyejifungua... maana watoto wa aliyeachwa watakuwa wengi zaidi kuliko watoto wa aliye na mume."


*MAOMBI YA SIKU YA PILI*
"Baba wa mbinguni, nakushukuru kwa siku hii ya pili ya maombi yangu. Asante kwa kuwa wewe ni Mungu wa miujiza na hakuna lisilowezekana kwako.

Nakuja mbele yako leo kwa unyenyekevu, nakuomba neema ya kuzaa. Kuanzia Kwenye Uchumi Wangu na tumbo langu naKata kila kizuizi cha kiroho, kimwili, na kisaikolojia kinachonizuia kupata Matokeo nayostaili .

Bwana Futa kila jina la utasa katika maisha yangu kwa damu ya Yesu.

Natangaza Biashara Yangu, uchumi Wangu, kazi yangu imefunguliwa Kwa Jina la Yesu nakata utasa Kwenye MIKONO yangu

Natangaza kuwa tumbo langu limefunguliwa kwa jina la Yesu. Ninaamini kuwa mwaka huu nitashuhudia wema wako kwa kupata mtoto wangu mwenyewe. Nipatie subira, amani, na nguvu ya kuendelea kungoja jibu lako.

Nashukuru kwa kuwa umenisikia. Kwa jina la Yesu Kristo, Amina."

---

Mtu wa Mungu Soma maandiko haya mara 3, halafu fanya maombi haya kwa moyo wote. Ikiwa unafurahi, andika alama ya "โœ๏ธ" hapa nikujue tuko pamoja kwenye siku ya tatu kesho.

3 weeks ago | [YT] | 2

YAWEZEKANA Tv

*BWANA YESU ASIFIWE WATUMISHI WA MUNGU KARIBUNI KATIKA MAOMBI YA SIKU 90 ZA MAOMBI YA MGEUKO MKUU KWENYE KILA ENEO LA MAISHA YAKO*


90 DAY 1
[ *MAOMBI YA SHUKRANI KWA BWANA* ]

Luka 17:17-19
[17] Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?

[18] Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?

[19] Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.

Zaburi 18:49
[49] Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

OMBA ๐Ÿ‘‡

Baba katika Jina la Yesu nimekuja mbele zako kwa moyo wa shukrani, nimekuja kukupa utukufu Mungu wangu nikiwa naanza Maombi Haya ya siku 90.

Asante kwa neema yako,umekuwa msaada wangu Mungu wangu na Baba yangu,asante kwa kibali na upendeleo wako kwangu katika miezi ilopita

Asante kwa kunikumbuka na kunipa Kibali Cha Kushiriki Kuomba

Hakika ni kwa neema yako umenikumbuka nami nanyenyekea naomba pokea shukrani za moyo wangu kwani sina Mungu mwingine zaidi yako Mungu wangu.

Moyo wangu umejawa sifa naomba utukuzwe Mungu anaetukamilisha

ENDELEA kuomba

3 weeks ago | [YT] | 2

YAWEZEKANA Tv

โ˜€๏ธ *MAOMBI YA KUIKABIDHI WIKI NA MWEZI MPYA MIKONONI MWA BWANA*โ˜€๏ธ

๐Ÿ™*MWEZI WA KUSHINDA KILA VITA* ๐Ÿ™

BABA wa Mbinguni, katika Jina kuu na lenye mamlaka la YESU KRISTO, ninakuja mbele Zako leo kwa moyo wa shukrani. Asante kwa kunivusha salama kutoka mwezi uliopita na kunipa neema ya kuuona mwezi huu mpya. Asante kwa pumzi ya uzima, kwa ulinzi Wako, kwa rehema Zako, na kwa wema Wako ambao haujaisha kamwe.

โœ๏ธ BWANA YESU, leo naiweka wiki hii na mwezi huu mpya mikononi Mwako.

๐Ÿฉธ Ninakukabidhi maisha yangu.
๐Ÿฉธ Ninakukabidhi familia yangu.
๐Ÿฉธ Ninakukabidhi afya yangu.
๐Ÿฉธ Ninakukabidhi kazi na biashara zangu.
๐Ÿฉธ Ninakukabidhi huduma yangu.
๐Ÿฉธ Ninakukabidhi mipango na malengo yangu yote.

Bwana, nenda mbele yangu ukanyooshe njia zilizopinda. Fungua milango ambayo hakuna mwanadamu awezaye kuifunga, na funga milango ambayo si mapenzi Yako kwangu.

๐Ÿ“– Zaburi 37:5
"Umkabidhi BWANA njia yako, pia umtumaini, naye atafanya."

โœ๏ธ Baba, mwezi huu natangaza kuwa ni mwezi wa kushinda kila vita.

โ–ช๏ธ Nitashinda vita vya kiroho.
โ–ช๏ธ Nitashinda vita vya kifedha.
โ–ช๏ธ Nitashinda vita vya afya.
โ–ช๏ธ Nitashinda vita vya familia.
โ–ช๏ธ Nitashinda vita vya hatima yangu.
โ–ช๏ธ Nitashinda kila hila ya adui iliyopangwa dhidi yangu.

Kwa damu ya YESU, natengua kila mpango wa giza, kila kikwazo, kila kucheleweshwa na kila nguvu ya adui iliyolenga kuzuia maendeleo yangu mwezi huu.

๐Ÿ“– Warumi 8:37
"Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda."

โœ๏ธ Ee Mungu Mwenye Nguvu, ninaomba ulinzi Wako juu yangu na familia yangu mwezi huu wote.

โ–ช๏ธ Tulinde na ajali.
โ–ช๏ธ Tulinde na magonjwa.
โ–ช๏ธ Tulinde na taarifa mbaya.
โ–ช๏ธ Tulinde na mashambulizi ya adui.
โ–ช๏ธ Tulinde katika kutoka na kuingia kwetu.

๐Ÿ“– Isaya 41:10
"Usiogope, maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia."

โœ๏ธ Baba, mwezi huu nipe neema ya kushinda kila changamoto nitakayokutana nayo. Mahali ambapo wengine watakata tamaa, nipe nguvu za kusonga mbele. Mahali ambapo milango imefungwa, nifungulie njia mpya. Mahali ambapo kuna vita, nipe ushindi.

โ˜€๏ธ Mwezi huu natangaza kwa imani:

โ–ช๏ธ Nitashinda kila vita.
โ–ช๏ธ Nitapokea ushindi katika kila eneo la maisha yangu.
โ–ช๏ธ Neema ya Mungu itanifuatilia.
โ–ช๏ธ Amani ya Mungu itanitawala.
โ–ช๏ธ Afya njema itakuwa sehemu yangu.
โ–ช๏ธ Mafanikio yatakuwa urithi wangu.
โ–ช๏ธ Ushuhuda mpya utatokea katika maisha yangu.

๐Ÿ“– Yeremia 29:11
"Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini na mwisho mwema."

โœ๏ธ Baba, ninaikabidhi wiki hii na mwezi huu wote mikononi Mwako. Utawale, uongoze, ubariki na uufanye kuwa mwezi wa ushindi, mwezi wa neema, mwezi wa mafanikio, na mwezi wa ushuhuda.

Ninaamini kwamba kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU, nitashinda kila vita na kuona wema Wako katika siku zote za mwezi huu.

๐Ÿ™ Katika Jina la YESU KRISTO nimeomba na kuamini.

๐Ÿ”ฅ AMEN! AMEN! AMEN! ๐Ÿ”ฅ

โœจ TANGAZO LA MWEZI:
"MWEZI HUU NITASHINDA KILA VITA, KWA JINA LA YESU!"

4 weeks ago | [YT] | 1

YAWEZEKANA Tv

Kila changamoyo inayo kukabili ๐Ÿ‘‡

1 month ago | [YT] | 5

YAWEZEKANA Tv

Makovu uliyo nayo

1 month ago | [YT] | 2

YAWEZEKANA Tv

๐— ๐—ช๐—ข๐—ก๐—š๐—ข๐—ญ๐—ข ๐—ž๐—ช๐—” ๐—”๐— ๐—•๐—”๐—ฌ๐—˜ ๐—›๐—”๐—๐—จ๐—œ ๐—ž๐—จ๐—ข๐— ๐—•๐—”

1๏ธโƒฃ:๐—ž๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐—บ๐—ฎ๐—ผ๐—บ๐—ฏ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—บ๐˜€๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐—ป๐—ฎ ๐—บ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐˜‚๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ (๐—ž๐˜‚๐—บ๐˜๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐˜‚๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐—บ๐—ฝ๐—ฎ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐—ต๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ถ๐—บ๐—ฎ)

Unapoanza kuomba, usianze haraka kuomba mahitaji yako,Anza kwa kumheshimu Mungu na kutambua ukuu wake. Mshukuru kwa uzima,ulinzi na mambo yote aliyokufanyia hata kama huyaoni yote waziwazi. Hii huandaa moyo wako kuwa katika unyenyekevu na imani mbele zake.

Mungu anapenda sifa,Anza maombi
yako kwa kumsifu Yeye ,Msifu kwa sifa zake zote,Taja sifa mbele za Mungu

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;Zaburi 100:4

2๏ธโƒฃ:๐—ง๐˜‚๐—ฏ๐˜‚ ๐—ฑ๐—ต๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ถ ๐˜‡๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ธ๐—ฎ๐—ฏ๐—น๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ
๐—ธ๐˜‚๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฒ๐—น๐—ฒ๐—ฎ

Maombi yenye nguvu huambatana na moyo unaotaka kutengenezwa. Kabla hujaomba mahitaji yako, muombe Mungu akusamehe makosa yako.

Toba humfanya mtu awe huru mbele za Mungu na huondoa mzigo wa hatia ndani ya moyo

Mungu anawapokea wale wanaorudi kwake kwa unyenyekevu. Mungu hupenda moyo wa toba

Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu.1 Yohana 1:9

3๏ธโƒฃ:๐—ข๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ท๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—น๐—ฎ ๐—ฌ๐—ฒ๐˜€๐˜‚ ๐˜†๐—ผ๐˜๐—ฒ
๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ๐˜†๐—ผ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐˜†๐—ฎ๐—ต๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ท๐—ถ

Usiombe kwa jina tofauti na Yesu
maana hilo ndilo tunapaswa kuomba
kwalo,Ukitaka kupokea omba kwa jina la
Yesu

Jina la Yesu lina mamlaka,ushindi,
uponyaji na nguvu dhidi ya kila nguvu
za giza

Yohana 14:13-14
[13]Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani
ya Mwana.
[14]Mkiniomba neno lo lote kwa jina
langu, nitalifanya.
Mathayo 7:7-8

4๏ธโƒฃ:๐—จ๐˜€๐—ถ๐—บ๐—น๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ธ๐—ถ๐—ฒ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ผ๐—บ๐—ฏ๐—ถ

Usimlaumu Mungu kwamba kwanini hili ?
Mungu kwanini hili limetokea Mbona unanionea Mungu

Kumlalamikia Mungu kutakufanya uache kuona wema wa Mungu na inakupunguzia imani kwake,Kulalamika kunaweza kukufanya umkatie Mungu tamaa

Nenda mbele za Mungu kwa hoja zenye nguvu na sio kulalamika ,Mwambie Mungu nini unahitaji be Clear and Specific

Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.
Isaya 41:21

5๏ธโƒฃ:๐—ข๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ฝ๐—ฒ๐—ป๐˜‡๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Ukiomba mapenzi ya Mungu yatimizwe unamruhusu Mungu akuongoze katika njia iliyo bora zaidi kuliko mawazo na hisia zako.

Mungu ndiye anayejua mwisho wa jambo kabla hata halijaanza,Kuomba mapenzi ya Mungu ni Ishara ya unyenyekevu kwamba Mungu anakupenda na anajua kilicho bora zaidi kwenye maisha yako kuliko hata wewe mwenyewe.

Ukiomba kitu nje na mapenzi ya Mungu huwezi kupokea ,Ukiomba sawa sawa na Mapenzi yake utapokea

1 Yohana 5:14,Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

6๏ธโƒฃ:๐—ข๐—บ๐—ฏ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—ถ๐—บ๐—ฎ๐—ป๐—ถ

Mungu anapendezwa na mtu mwenye
imani ,Usipokuwa na imani huwezi
kupokea mambo makubwa kutoka
kwake ,Hivyo lolote ambalo unaliomba
hakikisha unaamini kuwa tayari
umekwisha kupokea

Kama huwezi kuamini ni bora usiombe ,Ukiwa na imani kubwa
utapokea mambo makubwa

Kwa sababu hiyo nawaambia:
Mkiomba lolote kwa kuamini kwamba mmepokea, mtapewa
Marko 11:24,

7๏ธโƒฃ:๐— ๐˜„๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ถ๐—ฒ ๐—ฅ๐—ผ๐—ต๐—ผ ๐— ๐˜๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ณ๐˜‚ ๐—ฎ๐—ธ๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ฑ๐—ถ๐—ฒ ๐—ธ๐˜‚๐—ผ๐—บ๐—ฏ๐—ฎ

Kuna nyakati unataka kuomba lakini hujui uanzie wapi au useme nini mbele za Mungu. Wakati mwingine moyo huwa mzito kutokana na majaribu,huzuni na mawazo mengi

Hivyo ni muhimu kumuomba Roho Mtakatifu akusaidie kuomba

Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui
kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8:26

Mwezi wa 6,June kuanzia tar 1 hadi 7 tumekuandalia siku 7 za kufunga na
kuomba masaa 12 kila siku kuombea
mahitaji yetu na kujenga ushirika wetu
na Mungu na tutakuwa na muda wa kuombea mahusiano na ndoa zetu

Kama uko tayari jiunge nasi kwa ku comment neno MAOMBI

Kama umesoma mpaka mwisho
comment neno Amen na nisaidie kumtumia na mwenzako mjifunze kuomba pamoja

Share ili marafiki zako wajifunze kuomba
Save ili kesho urudi kujikumbusha

Mungu akubariki

1 month ago | [YT] | 2

YAWEZEKANA Tv

Mvumilivu hula Mbivu

1 month ago | [YT] | 5

YAWEZEKANA Tv

Elewa hii

1 month ago | [YT] | 7