Mojawapo ya mbinu za kimtindo ambayo mwandishi ametumia kwa mapana ni mbinu ya uwili. Uwili ni hali ambapo matukio au vitu hutokea viwiliviwili kimuktadha. Kuna uwezekano vitu hivyo vikatokea kisadfa au kimaksudi kutegemea na namna alivyonuia mwandishi. Familia mbili kuu zimetawala siasa za Matopeni kwa muda mrefu; familia ya Zuzu Matata na ile ya Mzee Sugu Senior. Wanaowania uongozi wa Matopeni ni wawili; Sugu Junior na Fumo Matata. Sugu Junior ametawala Jimbo la Matopeni kwa awamu mbili. Sasa hivi anajaribu kuwania kwa awamu ya tatu. Pale Matopeni kuna makundi mawili yanayokinzana kisiasa. Kwanza ni upande wa serikali na pili ni upande wa upinzani. Katika hali hii, serikali inajigamba namna ilivyofanya maendeleo huku upinzani ukipuuzilia mbali majigambo ya serikali. Hali kadhalika, kuna makundi mawili ya watu katika jamii ya Matopeni; wapiga kura ambao wanawakilishwa na akina Zuhura na Machoka kisha kuna viongozi wapigiwa kura ambao wanawakilishwa na akina Fumo Matata na Sugu Junior. Katika siasa, kuna masuala mawili; kupiga kura na kuhesabu kura. Hata hivyo, pale Matopeni kupiga kura si hoja, muhimu ni anayetangazwa mshindi baada ya kuhesabu kura hizo. Suala hili linaibua swali, kuna umuhimu gani kushiriki zoezi la kupiga kura? Jimbo la Matopeni limewahi kuwa na watawala wawili pekee yaani Sugu Senior na Sugu Junior. Aghalabu viongozi wengi wa kisiasa wa Matopeni wana majina mawili mawili; Fumo Matata, Sugu Senior, Sugu Junior na pia mhusika Kahindi Mlalama. Vilevile, shairi la Malenga Mteule lina beti mbili. Katika jamii hii pia kuna kundi la watu waliosoma na lile la watu ambao hawajasoma. Zuhura anasema watampa kura mtu wao awe amesoma au hajasoma, almradi ni wa kabila lao. Siku ya sherehe pale uwanjani Mamboleo kunadhihirika pande mbili; upande wa walalahoi ambao ni wa wapiga kura walioketi kwenye jua kali na ule mwingine ni wa wanasiasa ambapo pametundikwa hema kuwakinga dhidi ya ukali wa jua. Hili linaonyesha namna utabaka ulivyokithiri katika jamii hii. Matukio katika hadithi yanatokea katika vipindi viwili; kuna kipindi cha kwanza ambacho ni cha kampeni kisha kuna kipindi cha pili ambacho ni cha baada ya uchaguzi. Wakati wa kampeni, wanasiasa wanatagusana na wananchi, baada ya uchaguzi kunajengeka ukuta kati yao, inakuwa vigumu hata kumkaribia mwanasiasa.
Wasiliana nami kupitia 0712366932 kwa maongezi ya MAANDALIZI YA KCSE shuleni mwako
Brian Witkins
Majaliwa kesho #KCSE2023
2 years ago | [YT] | 2
View 0 replies
Brian Witkins
Hivi karibuni ndani ya West TV dawati la lugha na YouTube channel Brian Witkins
2 years ago | [YT] | 1
View 0 replies
Brian Witkins
Mojawapo ya mbinu za kimtindo ambayo mwandishi ametumia kwa mapana ni mbinu ya uwili. Uwili ni hali ambapo matukio au vitu hutokea viwiliviwili kimuktadha. Kuna uwezekano vitu hivyo vikatokea kisadfa au kimaksudi kutegemea na namna alivyonuia mwandishi.
Familia mbili kuu zimetawala siasa za Matopeni kwa muda mrefu; familia ya Zuzu Matata na ile ya Mzee Sugu Senior.
Wanaowania uongozi wa Matopeni ni wawili; Sugu Junior na Fumo Matata.
Sugu Junior ametawala Jimbo la Matopeni kwa awamu mbili. Sasa hivi anajaribu kuwania kwa awamu ya tatu.
Pale Matopeni kuna makundi mawili yanayokinzana kisiasa. Kwanza ni upande wa serikali na pili ni upande wa upinzani. Katika hali hii, serikali inajigamba namna ilivyofanya maendeleo huku upinzani ukipuuzilia mbali majigambo ya serikali.
Hali kadhalika, kuna makundi mawili ya watu katika jamii ya Matopeni; wapiga kura ambao wanawakilishwa na akina Zuhura na Machoka kisha kuna viongozi wapigiwa kura ambao wanawakilishwa na akina Fumo Matata na Sugu Junior.
Katika siasa, kuna masuala mawili; kupiga kura na kuhesabu kura. Hata hivyo, pale Matopeni kupiga kura si hoja, muhimu ni anayetangazwa mshindi baada ya kuhesabu kura hizo. Suala hili linaibua swali, kuna umuhimu gani kushiriki zoezi la kupiga kura?
Jimbo la Matopeni limewahi kuwa na watawala wawili pekee yaani Sugu Senior na Sugu Junior.
Aghalabu viongozi wengi wa kisiasa wa Matopeni wana majina mawili mawili; Fumo Matata, Sugu Senior, Sugu Junior na pia mhusika Kahindi Mlalama.
Vilevile, shairi la Malenga Mteule lina beti mbili.
Katika jamii hii pia kuna kundi la watu waliosoma na lile la watu ambao hawajasoma. Zuhura anasema watampa kura mtu wao awe amesoma au hajasoma, almradi ni wa kabila lao.
Siku ya sherehe pale uwanjani Mamboleo kunadhihirika pande mbili; upande wa walalahoi ambao ni wa wapiga kura walioketi kwenye jua kali na ule mwingine ni wa wanasiasa ambapo pametundikwa hema kuwakinga dhidi ya ukali wa jua. Hili linaonyesha namna utabaka ulivyokithiri katika jamii hii.
Matukio katika hadithi yanatokea katika vipindi viwili; kuna kipindi cha kwanza ambacho ni cha kampeni kisha kuna kipindi cha pili ambacho ni cha baada ya uchaguzi. Wakati wa kampeni, wanasiasa wanatagusana na wananchi, baada ya uchaguzi kunajengeka ukuta kati yao, inakuwa vigumu hata kumkaribia mwanasiasa.
Wasiliana nami kupitia 0712366932 kwa maongezi ya MAANDALIZI YA KCSE shuleni mwako
2 years ago | [YT] | 5
View 1 reply
Brian Witkins
Jipe Nakala yako leo. Wasiliana nami kupitia 0712366932.
2 years ago | [YT] | 3
View 1 reply
Brian Witkins
Siku ya kiswahili duniani. Kiswahili fahari yangu
2 years ago | [YT] | 5
View 0 replies
Brian Witkins
Kiswahili ni lugha halisi ya Afrika. Iwapo Afrika inataka kujikwamua kutoka kwenye ubeberu na ukoloni Mambo leo,basi hatuna budi ila tuikuze lugha hii yenye asili yetu! @kakafred5028 @HiranMugaisi @dalmussakali9921 @KauleniTVKe
3 years ago | [YT] | 5
View 0 replies
Brian Witkins
Ni wakati mwingine tena watahiniwa wanaukalia mtihani wa kitaifa wa KCSE. Wiki kesho Jumatano na Halhamisi ni karatasi ya kiswahili 102.
Kila la heri kwa watahiniwa wote. Tunatarajia matokeo mazuri katika kiswahili.
3 years ago | [YT] | 4
View 0 replies
Load more