MAFINGA CATHOLIC TV 💒📸🎥 ni Kitalu kilichoanzishwa kwa ajili ya kutangaza Neno La Mungu Kwa Watu.
Ni channel inayokuletea matukio yote ya kanisa katoliki yakiwemo Misa Takatifu, Upadrisho, Ushemasi , Jubilei, Safari Za Miito Mitakatifu, Fahamu Za Biblia Takatifu, Vitabu vya kiroho...N.k
Unapoitembelea channel yetu Tafadhari #SUBSCRIBE, LIKE ,COMMENT NA SHARE kwa ndugu ,jamaa na marafiki ili utume wetu ukue na kuwafikia wengi.
MAFINGA CATHOLIC TV......... Sauti ya Injili 📸🎥....
For Bookings👇👇👇👇
CONTACTS US :: 0750903616// 0620785527.
Follow Us On 👇👇👇👇👇
INSTAGRAM; #Mafinga Catholic
FACEBOOK; #Jimbo Katoliki Mafinga
Lakini pia tumeandaa group la WhatsApp litakalokuwezesha kupata taarifa za Matukio mbalimbali ya Kanisa Muda Wote ... Kama ungependa kuwa mmoja wetu ..Unaweza kujiunga kwa hiari Kupitia Link hii 👇👇👇👇na Mungu Akubariki
chat.whatsapp.com/CjAu45Pdn1W4HVahVYUsQf
Mafinga Catholic TV
1 month ago | [YT] | 6
View 1 reply
Mafinga Catholic TV
MASOMO YA MISA, MACHI 6, 2023
JUMATATU, JUMA LA 2 LA KWARESIMA
SOMO 1
Dan. 9:4 – 10
Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.
Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi. Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 79:8 – 9, 11, 13 (K) 103:10
(K) Usitutende sawasawa na hatia zetu, Ee Bwana.
Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako zije kutulaki hima,
Kwa maana tumedhilika sana. (K)
Ee Mungu wokovu wetu utusaidie.
Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,
Kwa ajili ya jina lako. (K)
Kuugua kwake aliyefungwa na kuingia mbele zako.
Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako.
Uwahifadhi wana wa mauti.
Na sisi tulio watu wako, na kondoo za malisho yako,
Tutakushukuru milele;
Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi. (K)
SHANGILIO
Mt. 4:4
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
INJILI
Lk. 6:36:38
Yesu aliwaambia wafuasi wake: Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. Wapeni watu kitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifruani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
3 years ago | [YT] | 11
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatatu, Machi 6, 2023
Juma la 2 la Kwaresima
Dan 9:4-10
Zab 79:8-11,13
Lk 6:36-38
USIHUKUMU!
Ulishawahi kukutana na mtu kwa mara ya kwanza na bila hata kuongea na huyu mtu mara moja unahitimisha unayofikiri juu yake au wao? Kama sisi wenyewe ni waaminifu ni lazima tukiri kwamba ni rahisi kuhukumu watu wengine kwa haraka. Kilicho kigumu ni kubadilisha hukumu yetu tuliojiwekea kuhusu hao wengine. Ni vigumu kuwahukumu tukiwapa mafanikio na kuondoa wasi wasi wetu na kufikiri ni wazuri.
Yesu alivyosema “usihukumu nawe hauta hukumiwa” anatualika sisi tusiwe watu wa kuwahukumu watu katika hali yeyote. Ulimwengu unahitaji watu wengi wasio hukumu na wala kulaani. Tunahitaji watu wanao fahamu kutengeneza urafiki na kuleta upendo usio na masharti. Na Mungu anataka wewe uwe mmoja wao wa hao watu. Tutafakari ni mara ngapi tumekuwa watu wakuwahukumu watu, na tutafakari ni kwa namna ghani sisi ni wazuri katika kutengeneza urafiki na wale wote walio karibu yetu. Mwishowe, kama tumekuwa watu wa kutengeneza huu urafiki, ni wazi tutapokea Baraka kutoka kwa wengine wanao tupatia na sisi urafiki kama huo. Na kwa njia hiyo sisi wote tutabarikiwa.
Sala: Bwana, ninaomba unipe moyo usio hukumu. Ninaomba unisaidie niwapende wote ninao kutana nao kwa mapendo matakatifu na kuwakubali. Ninaomba unipe mapendo ya kweli na urafiki wa kweli kwa wengine ili niweze kuamini na kufurahia upendo unaopenda mimi niwe nao. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
3 years ago | [YT] | 8
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
*Mtakatifu Colette Mtawa*
Mtakatifu Colette alizaliwa tarehe 13 Januari 1380, huko Corbie, Burgundy Ufaransa. Alibatizwa na kuitwa Nicolette, lakini walimuita Colette.
Akiwa na miaka 17,wazazi wake walikufa. Akagawa urithi wake kwa maskini, akajiunga na watawa wa Franciscan.
Mwaka 1406 alipata wazo la kuanzisha shirika la watawa la Poor Clares. Kwa baraka za Papa Benedict XIII, alifanikiwa kuanzisha nyumba 17 katika sehemu tofauti.Na yeye mwenyewe akaishi katika Convent ya Ghent.
Mtakatifu Colette, alikufa mwaka 1447 March 6, huko Ghent, akatangazwa mwenye heri mwaka 1740 januari 23 na Papa Clement XII, na akatangazwa mtakatifu mwaka 1807 May 24 na Papa Pius VII.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Baldred
Mt. Balther
Mt. Basil
Mt. Bilfrid
Mt. Cadroe wa Metz
Mt. Conon
Mt. Evagrius wa Constantinople
Mt. Fridolin
Wt. Kyneburga, Kyneswide, na Tibba
Mt. Marcian wa Tortona
Mt. Ollegarius
*Mtakatifu Colette, Wenyeheri na Watakatifu wengine wote wa leo , Mtuombee*
3 years ago | [YT] | 5
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
MASOMO YA MISA, MACHI 5, 2023
JUMAPILI YA 2 YA KWARESIMA
SOMO 1
Mwa. 12:1 – 4a
Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulitukuza jina lako; nawe uwe Baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 33:4 – 5, 18 – 20, 22 (K) 22
(K) Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda haki na hukumu,
Nchi imejaa fadhili za Bwana. (K)
Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)
Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe. (K)
SOMO 2
2Tim. 1:8b – 10
Uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Mt. 17:5
Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.”
INJILI
Mt. 17:1 – 9
Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohane nduguye, akawaleta juu yam lima mrefu faraghani; akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
Petro akajibu akamwambia Yesu, Bwana, ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya hapa vibanda vitatu, kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye. Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope. Wakainua macho mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu yeyote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
3 years ago | [YT] | 5
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumapili, Machi 5, 2023.
Dominika ya 2 ya Kwaresima
Mwa 1:1-4;
Zab 33:4-5, 18-22;
2 Tim 1:8-10;
Mt 17: 1-9.
KWARESIMA: MUDA WA KUMFAHAMU YESU!
Juma la kwanza la Kwaresima linatuandaa, kufanya matendo ya kwaresima, kusali, kufunga na kutoa sadaka. Inakuwa ni hatua kwetu kutengeneza hali nzuri ya kuingia katika kipindi hichi kwa undani. Jumapili iliopita ilituandaa kuhusu majaribu, na umuhimu wa kusafisha dhambi zetu rohoni mwetu. Yesu alituanyesha njia ya kumshinda shetani na dunia na pia vishawishi vya miili yetu, alipokuwa jangwani. Leo anajifunua kwa njia ya Kugeuka sura kutualika wote kwenye utukufu alio nao na Baba yake. Kwa njia ya kungara sura tunaalikwa kwenye ufufuko wa miili, wakati tutakapo kuwa huru kuhusu dhambi. Kama mwili wa Yesu ulivyokuwa katika utukufu, ndivyo miili ya watakatifu itangaa. “Utukufu ulionipa mimi nimewapa wao” (Yn 17:22).
Uhusiano unakuwa kadiri ya muda. Tunawafahamu watu zaidi kadiri ya muda unavyo sogea. Mitume pia lazima na wao waliendelea kumfahamu Yesu kadiri ya muda ulivyokuwa ukisogea. Uhusiano wao ulianza alivyo waita hapo awali. Waliishi naye na kumsikiliza na kushuhudia miujiza na uponyaji mbali mbali. Uelewa wao lazima utakuwa ulikuwa kadiri ya muda, mpaka Petro akafikia kiwango cha kusema “Wewe ni Masiha Mwana wa Mungu aliye hai”. Lakini Petro alimpinga alivyosikia habari ya kifo chake, na Yesu alitambua kuwa Wafuasi wake hawajamfahamu vizuri bado. Walimwelewa vibaya kuwa kama Masiha wa kidunia atakaye iongoza dunia daima. Ndio, maana baada ya siku sita hivi Yesu awaliwachagua Petro, Yohane na Yakobo kwenda mlima na kushuhudia kungara kwake kwa sura inayoelezewa leo katika Injili.
Kungara sura kwa Yesu kunatokea wakiwa juu ya milima. Mlimani palijulikna kama sehemu ya kukutana na Mungu. Wakati Yesu anageuka sura mavazi yake yalingaa sana na uso wake ulingara. Taswira hii alioionyesha Yesu ni hali ya utukufu ambayo itakuja baada ya maisha ya ulimwengu huu. Musa na Elia ambao katika tamaduni ya Wayahudi waliwakilisha mambo mawili muhimu ya Wayahudi. Sheria na Manabii. Musa na Elia walikuwa ni watu ambao walipata kuwasiliana na Mungu wakiwa katika milima. Na waliwaongoza watu wa Israeli kumrudia Mungu.
Kwa kuangalia hali hii ya kugusa na kuogopesha, Petro anaomba kujengwe vibanda vitatu kimoja cha Yesu, kimoja cha Elia na kimoja cha Musa. Petro alipenda hii hali iendelee kuwapo. Mungu anaingia kati na kumfunua mwanae (Mwana wa Mungu) kwa wafuasi “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa…” Mitume wanaogopa na wanainamisha nyuso zao. Walivyo nyanyuka walikuta kila kitu kikiwa katika hali yakawaida. Tukio hili ni lazima lilikuwa ni la nguvu sana kuliko tukio lolote lile ambalo mitume hawa watatu waliweza kulishuhudia. Katika tukio hili la kungara sura, Umungu wa Yesu ulifunuliwa kwao. Waliweza kufahamu Yesu ni nani na kwanini Yesu alikuwa akiongelea kuhusu kifo na ufufuko . wafuasi waliweza kuja kumfahamu Yesu vizuri zaidi wakati wa Karamu ya mwisho, mateso yake alivyokuwa pale Getsemane, mateso yake, kifo na kufufuka. Muda wote waliokuwa na Yesu waliweza kuja kumfahamu Yesu na kutambua nini maana ya kuwa wafuasi. Nasi ni hivyo hivyo.
Katika somo la kwanza tunasikia kuhusu kuitwa kwa Abrahamu. Abrahamu anajibu wito wa kwanza kabisa wa Mungu. Na ni baada ya muda tu alikuja kumfahamu Mungu vizuri na utume wake kwa ajili yake. Hivyo, tunavyopata muda wa kuwa na Mungu zaidi ndivyo tunavyozidi kuendelea kumfahamu zaidi, na kadiri tunayo endelea kumfahamu Mungu, ndivyo tunavyo fahamu mpango wake kwetu.
Kwaresima ni kipindi cha kutafakari na kukaribisha neema ya Mungu katika maisha yetu. Sio muda tu wakuachia vitu, bali pia ni muda wakupokea zawadi kubwa kutoka kwa Mungu. Mungu hajatusahau sisi watoto wake ila ni sisi tuliomsahau yeye na kukimbia uso wake. Leo, upendo unafunuliwa kwetu kwa njia ya Yesu. Yesu kwa njia ya ufufuko anatufanya sisi kuwa sehemu ya mpango wa Mungu tangu milele, kuwa watakatifu na kupendwa na Mungu kwa kuwa daima mbele zake. Ufufuko unaleta kwetu mwanga katika maisha yetu kama wa kungara sura kwa Yesu, kiasi kwamba hakuna giza linalo baki.
Maandiko matakatifu yanatuonesha njia ya kwenda katika muelekeo huu. Kwanza kabisa, kuwa na muda wa kusali kama Yesu. Pili ni kumfahamu Yesu, na hili linafanyika kwa kutafakari Maandiko Matakatifu, Mungu aliwaambia wafuasi kwamba “Msikilizeni yeye” pia Neno la Mungu linafunua nafsi ya Yesu kwetu sisi kila siku. Tatu, tuwe tumeungana katika jumuiya zetu. Kama mitume watatu walivyo pata kumshuhudia Yesu, na kushiriki katika mwanga uliofunuliwa na Mungu. Hili linawezekana daima tunavyo shiriki katika Ekaristi Takatifu, tunaitwa wote kuunganika katika kungara kwa Yesu katika Ekaristi takatifu. Na mwisho kabisa, kushiriki katika mahusiano mazuri na wenzetu. Mitume hawakuweza kushirikisha walio yaona muda ule, bali walishirikisha baada ya ufufuko wakati wamesha elewa maana kamili ya kungara kwake sura, walishirikisha wengine kwa kuhubiri habari Njema. Sisi pia tunaitwa kutangaza kungara kwa sura kwa Yesu kwa kuwatangazia wale wote waliotengwa. Tunaitwa kutambua matendo ya roho na matendo ya nje ya huruma: kuwalisha maskini, kuwapa maji walio na kiu, kuwavisha wasio na nguo, kuwakaribisha wasio na makao, kuwaponya wagonjwa, kutembelea wafungwa, kuwazika wafu, , kuwasaidia walio na mashaka, kuwaelekeza walio wajinga, kuwa elekeza wadhambi warudi, kuwafariji wenye matatizo, kuwasamehe walio tukosea, kuchukuliana kwa huruma wale wote wanao tuumiza na kuwaombea walio wazima na wafu.
Sala: Bwana, ninaomba nifarijike kwa utukufu wako na ukweli wako. Ninaomba nikumbuke utukufu huu ninapo tembea katika changamoto mbali mbali katika maisha. Utatembea mbele yangu na kunitangulia nikikuamini wewe. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
3 years ago | [YT] | 4
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
MTAKATIFU JOHN JOSEPH, PADRI
5 MACHI
Mama Kanisa anatualika kumkumbuka Mtakatifu John Joseph aliyezaliwa mwaka 1654 katika kisiwa cha Ischia,karibu na Naples, Italia.
Akiwa na miaka 16 tu, alijiunga na shirika la Wa Franciscan. Miaka 3 tu baadaye alitumwa kwenda kuanzisha monasteri huko Piedmont. Baada ya kusoma, alipata daraja la upadri.
Kwa idhini ya wakuu wake wa shirika, alijenga monasteri nyingine ambayo hata hivyo mwaka 1702 ,aliiacha, baada ya mgawanyiko wa majimbo kati ya Italia na Hispania.
Baada ya maangaiko, alifanikiwa kujenga manosteri nyingine ikiwa ni sehemu ya shirika lililobaki Hispania.
Mtakatifu John Joseph alikufa mwaka 1734 March 5, huko Ischia, Naples Italia.
Akatangazwa mwenye heri mwaka 1789 24 May na Papa Pius VI. Akatangazwa mtakatifu mwaka 1839 May 29 na Papa Gregory XVI.
Pia Kanisa linawakumbuka Watakatifu:
Mt. Adrian
Mt. Caron
Mt. Carthach wa Elder
Mt. Colman wa Armagh
M/h. Dionysius Fugishima
Mt. Eusebius wa Cremona
Mt. Gerasimus wa Jordan
Mt. Kieran wa Saigir
Mt. Oliva
Mt. Phocas wa Antioch
Mt. Piran
Mt Theophilus
Mt. Virgilius wa Arles
Mtakatifu John wa Msalaba, Utuombee!
3 years ago | [YT] | 4
View 1 reply
Mafinga Catholic TV
MASOMO YA MISA, MACHI 4, 2023
JUMAMOSI JUMA LA 1 LA KWARESIMA
SOMO 1
Kumb. 26:16-19
Musa aliwaambia watu: Leo hivi akuamuru Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na roho yako yote.
Umemwungama Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake, na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake; naye Bwana amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya kwa sifa, na jina na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako, kama alivyosema.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:1-2, 4-5, 7-8
(K) Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Heri walio kamili njia zao,
Waendao katika sheria ya Bwana.
Heri wazitiio shuhuda zake,
Wamtafutao kwa moyo wote. (K)
Wewe umetuamuru mausia yako,
Ili sisi tuyatii sana.
Ningependa njia zangu ziwe thabiti,
Nizitii amri zako. (K)
Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,
Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako.
Nitazitii amri zako,
Usiniache kabisa. (K)
SHANGILIO
Amo. 5:14
Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi, hivyo Bwana, atakuwa pamoja nanyi.
INJILI
Mt. 5:43-48
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yetu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu? Hata watoza ushuru; je! Nao hawafanyi yay ohayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
3 years ago | [YT] | 3
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Jumamosi, Machi 4, 2023
Juma la 1 la Kwaresima
Kumb 26: 16-19;
Zab 119: 1-2, 4-5, 7-8;
Mt 5: 43-48
KUTAMANI KUWA MKAMILIFU!
Liturujia ya leo inalenga katika Sheria ya Mungu, ambayo Mungu ametupa kwa njia ya Musa ili kuifuata kwa moyo na nafsi nzima. Katika Injili, tunaona Yesu, analeta upendo wenye athari kubwa, zaidi kuliko wowote ule ambao waliutenda kabla. Kumpenda kila mtu, bila kuwa na fikra au sababu yeyote ile, bila kujali kama wao wanatupenda sisi au la, bila kufikiria wanatuwazia mabaya au mazuri?
Yesu wakati alipokuwa dunia hii, alikabiliwa na upinzani sana, kutoka kwa mamlaka ya kidini, kutoka kwenye mamlaka ya kisiasa, kutoka mji wake mwenyewe, kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe. Hata hivyo, yeye amewapenda daima wote. Ujumbe wake wa huruma au wa kubadilika mara zote ulijawa na upendo mkuu. Hata juu ya Msalaba, aliwatazama kwa huruma watesi wake. Upendo kwa Mungu na kwa jirani huenda pamoja, na hauwezi kutenganishwa. Mt. Yohane anaweka wazi kwamba, “Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo (1Yoh 4:20).
Leo tunapewa changamoto na upendo huu wa Yesu Kristo. Tumekuwa mara nyingi sana watu ambao tunabagua wengine, juu ya rangi, dini, jinsia, kabila, juu ya tabaka, utaifa, juu ya hadhi ya jamii, utamaduni, elimu, kiasi cha mali ulicho nacho nk, Je, tunaweza kuamua kumwiga Yesu kuanzia sasa na kuendelea? Je, tunaweza kuwapenda wale wote ambao wametuumiza katika maisha yetu? Wale wanaotutesa kwasababu ya utamaduni wetu, dini yetu,au mawazo yetu? Yesu alishinda haya yote kwa upendo wake, Je, sisi twaweza kufanya hivyo tushinde kwa njia ya upendo?
Sala: Bwana, ninataka kuwa mtakatifu. Ninataka kuwa mtakatifu kama wewe ulivyo mtakatifu. Nisaidie niishi kila wakati kwa ajili yako. Ninatoa muda wangu wote kwa ajili yako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
3 years ago | [YT] | 0
View 0 replies
Mafinga Catholic TV
*Mtakatifu Casimir wa Poland*
Mtakatifu Casimir alizaliwa mwaka 1458 Oktoba 3 huko Wawel, Krakow- Poland.Alikuwa mwana wa mfalme Casimir IV wa Poland.
Mtakatifu Casimir tokea akiwa mdogo alimpenda Mungu, na alitambua kuwa maisha katika kasri ya kifalme, hayakuwa yake. Aliamua kuwa analala chini, na kula chakula cha kawaida.
Alikataa nyadhifa zote alizopewa, na akakataa pia kiti cha ufalme.Alikataa pia kuoa. Mambo hayo yalimgombanisha mno na baba yake.
Mtakatifu Casimir aliugua mapafu , na akafa mwaka 1484, Marchi 4, huko Hrodna, Lithuania.
Alitangazwa mtakatifu mwaka 1521 na Papa Leo X
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Adrian
Mt. Appian
Mt. Basil na wenzake
Mt. Basinus
Mt. Felix wa Rhuys
M/h. Humbert
Mt. Lucius I
Mt. Owen
Mt. Peter wa Pappacarbone
Mt. Placide Viel
*Mtakatifu Casimir, Wenyeheri na Watakatifu wengine wote wa leo, Mtuombee*
3 years ago | [YT] | 0
View 0 replies
Load more