Focus News Tanzania Tv 1, ni channel yako ya TV ya kiganjani ambapo utapata habari mbalimbali ikiwemo habari za kijamii, Siasa, Michezo na Burudani bila kusahau mahojiano katika mada mbalimbali.
Tupo Dodoma Makao Makuu ya Tanzania maeneo ya Ipagala jirani na kanisa la kwa Evance. Jiunge nasi kwa kubonyeza mandishi mekundu yaliyoandikwa Subscribe na kisha bonyeza alama ya kengere na hapo utakuwa umeungana nasi mubashara.
Akhsante kwa kuendelea kuichagua Focus News Tanzania kuwa channel yako pendwa ya TV ya kiganjani.
Focus News Tanzania Tv 1,
Mobile:.+255755834996
Whatsapp:β¦.+255755834996
E-mail:...focusnewsroomtanzania@gmail.com
Focus News Tanzania Tv 1
#LIVE: UHISPANIA V/S UBELGIJI HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA
Uhispania na Ubeligiji wanaingia dimbani kukabiliana uso kwa uso huku kila timu ikitaka kuibuka na ushindi na hataimaye kutinga hatua ya nusu fainali. Jana Alhamisi tulishuhudia Ufaransa ikitinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuwafunga mabao mawaili kwa bila Moroco katika moja ya nusu fainali ya kuvutia kabisa.
Ni yangu matumaini hujambo mpenzi mtazamaji wa Focus News Tanzania TV 1, Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya kuwania kombe la dunia hatua ya robo fainali, ambapo hivi punde tunakwenda kushuhudia moja ya mechi ambayo bila shaka itakuwa ni ya kukata na shoka baina ya Uhispania na Ubeligiji, mechi itakayopigwa katika Uwanja wa SoFi (SoFi Stadium), ambao kwa sasa unajulikana kama Uwanja wa Los Angeles kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.
ππππππππ
https://youtu.be/kzHxaEj4trI
16 hours ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
LIVE:CHADEMA WANAZUNGUMZA, MNYIKA ANAJIBU MASWALI MAGUMU
ππππππππ
https://youtu.be/1JB-3lE1xq0
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
JE HII NI NJIA YA TRUMP KUJIPATIA HURUMA NA UUNGWAJI MKONO NCHINI MAREKANI?
Gazeti la The Wall Street Journal linaripoti kuwa Israel imeipatia Washington taarifa zinazoonesha kuwa Iran inazingatia mpango mpya wa kutaka kumuua Donald Trump.
Taarifa hizi zinaonekana kuathiri mtazamo wa Rais wa Marekani zaidi kuliko hapo awali.
Katika siku za hivi karibuni, Trump amezungumzia hadharani vitisho vya kuuawa kwake mara kadhaa, akisema: "Wanataka kumuondoa kiongozi wa Marekani, yaani mimi," na "Jina langu liko kwenye orodha zao zote."
Taarifa hizi ambazo Israel ilimpa Trump, pamoja na jaribio lililoshindwa la kutaka kumuua huko Pennsylvania mnamo Julai 2024, ambalo Donald Trump anadai lilikuwa mpango wa Jamhuri ya Kiislamu, zimemfanya rais huyo wa Marekani kubadilisha suala hilo la jaribio la mauaji kutoka kuwa suala la kiusalama tu na kulifanya kuwa sehemu ya simulizi yake ya kisiasa.
ππππππππ
https://youtu.be/nM3E4_V8NZI
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
WATU 130 WAKAMATWA TANZANIA KWA TUHUMA ZA KUPANGA VURUGU ZA JULAI 7
Jeshi la Polisi Tanzania limesema linawashikilia watu 130 wanaotuhumiwa kuhusika katika kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu Julai saba mapema wiki hii.
Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, jeshi hilo limesema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia uchunguzi uliofanywa baada ya tahadhari za usalama zilizotolewa Juni 19 na Julai 5 mwaka huu.
Polisi wamesema uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watuhumiwa walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine kuhamasisha watu kushiriki katika vitendo vinavyokiuka sheria.
Taarifa hiyo imeorodhesha vitendo vinavyodaiwa kupangwa kuwa ni pamoja na kupanga, kutamka, kuandaa na kusambaza taarifa za uchochezi, kuhamasisha wananchi kushiriki katika vitendo vya kihalifu vinavyoweza kusababisha madhara kwa raia, kuchoma moto, kulipua transfoma za umeme, kuharibu miundombinu ya umma na mali za watu binafsi, pamoja na kushambulia askari wa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupora silaha.
πππππππππ
https://youtu.be/61DKVdWOq4o
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IRAN YASEMA MASHAMBULIZI MAPYA DHIDI YA MAENEO YA MAREKANI NI JIBU KWA MASHAMBULIZI YA USIKU KUCHA
Shirika la habari la Mehr, linalohusishwa na serikali ya Iran, limesema kuwa Iran imeanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya malengo ya Marekani ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Marekani yaliyofanywa usiku kucha katika maeneo ya kusini mwa Iran.
Kwa mujibu wa Mehr, maeneo ya Marekani nchini Kuwait yamelengwa kwa mashambulizi ya makombora yaliyofyatuliwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Shirika hilo pia limeripoti mashambulizi ya makombora dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Jordan, ambapo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, makombora manane yalitunguliwa ndani ya anga la nchi hiyo.
Aidha, milipuko imeripotiwa katika Victory Base mjini Baghdad, Iraq.
Wakati hayo yakichomoza tunaarifiwa ya kwamba, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kuwa vikosi vya Iran vimeweka chini ya udhibiti wao Mlango wa Bahari wa Hormuz (Strait of Hormuz).
πππππππππ
https://youtu.be/MRVeC4JgrTw
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
RAIS SAMIA ATOA ONYO KALI βHATUTASITA KUTUMIA DOLA KWA WATAKAOFANYA VURUGU NA VITENDO VYA KIGAIDI.β
Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan ametoa onyo kali kwa wale wote watakaojaribu kufanya vitendo vya kigaidi ili kuleta vurugu na uvunjifu wa amani nchi Tanzania kuwa watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria.
Rais Samia ameyasema hayo huko Zanzibar wakati wa tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa baina ya chama cha CCM na ACT Wazalendo Zanzibar.
βNiwaonye kwa mara nyingine wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kigaidi, kwamba taifa lolote duniani hutumia nguvu ya dola kuhami raia wake na kulinda heshima yake nasi Tanzania kama taifa hatutasita kufanya hivyo.β Amesema Rais Samia.
πππππππππ
https://youtu.be/fPo7jSyRzx4
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IRAN YADOKEZA KENYA NA NIGERIA HUENDA ZIKAHUSIKA KIJESHI KATIKA MZOZO WAKE NA MAREKANI
Kituo cha habari cha serikali ya Iran, IRIB, kimechapisha ujumbe kwenye mtandao wa X ukidai kuwa Kenya na Nigeria zina akiba za kimkakati za kijeshi ambazo zinaweza kutumika kwa wakati unaofaa.
Katika chapisho hilo, IRIB iliandika: βKenya na Nigeria pia zina akiba za kimkakati za kijeshi ambazo zitaingia uwanjani kwa wakati unaofaa.β
Hata hivyo, chapisho hilo halikutoa maelezo yoyote kuhusu akiba hizo za kijeshi, wala halikufafanua jinsi nchi hizo mbili zinavyodaiwa kuhusika katika mzozo unaoendelea.
πππππππ
https://youtu.be/1ksnPZPGkZ0
1 day ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
IRAN YAWASILISHA MALALAMIKO KWA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUPINGA MASHAMBULIZI YA MAREKANI
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema imewasilisha barua za malalamiko kwa Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufuatia mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani.
Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Saeed Iravani, amesema Marekani imeanzisha tena "mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya mamlaka na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," akidai kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa wazi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa pamoja na wajibu wake chini ya sheria za kimataifa.
Iravani pia alisema mashambulizi hayo yanakiuka kifungu cha makubaliano ya hati ya Maelewano ya Islamabad iliyosainiwa kati ya Iran na Marekani.
πππππππππ
https://youtu.be/zCBfSk_NOX4
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
WIZARA YA AFYA YA IRAN: WATU 14 WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIZI YA MAREKANI YA USIKU MBILI
Wizara ya Afya ya Iran imesema watu 14 wamefariki dunia katika duru hii ya hivi karibuni ya mashambulizi ya Marekani.
Kwa mujibu wa Hossein Kermanpour, mkuu wa kitengo cha mahusiano ya umma wa wizara hiyo, mashambulizi ya Marekani yaliyolenga majimbo matano nchini Iran tarehe 8 na 9 Julai pia yamesababisha watu 78 kujeruhiwa.
Kati ya majeruhi hao, watu 47 bado wamelazwa hospitalini wakipatiwa matibabu, aliongeza.
Wakati huo huo, gavana wa Iranshahr, wilaya iliyoko kusini mwa Iran, ameiambia vyombo vya habari vya serikali kuwa mtu mmoja aliuawa katika shambulizi la Marekani lililolenga jengo lililopo ndani ya uwanja wa ndege wa eneo hilo.
Marekani imeanzisha wimbi jipya la mashambulizi ya anga dhidi ya Iran, huku milipuko ikiripotiwa katika maeneo ya kusini mwa nchi, ikiwemo karibu na Bandar Abbas na maeneo mengine ya pwani.
Maafisa wa Marekani wamesema mashambulizi hayo yanalenga kupunguza uwezo wa Iran wa kutishia usafiri wa majini katika Mlango bahari wa Hormuz, kufuatia mashambulizi yaliyodaiwa kufanywa na Iran dhidi ya meli za kibiashara.
πππππππ
https://youtu.be/4zPFoMLBxb8
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Focus News Tanzania Tv 1
TRUMP ATISHIA MASHAMBULIZI ZAIDI DHIDI YA IRAN HUKU TEHRAN IKIONYA KUWA ITAJIBU βBILA WOGAβ
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba makubaliano ya usitishaji mapigano na Iran βyamekwishaβ, akiwashambulia viongozi wa nchi hiyo kwa kuwaita βwachafuβ na βwenda wazimuβ baada ya mashambulizi mapya ya usiku kucha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Nato nchini Uturuki, rais huyo wa Marekani alisema kuwa Marekani βiliwashambulia kwa nguvu sana jana usikuβ na kwamba βhuenda ikawashambulia tena kwa nguvu usiku wa leoβ.
Aliishutumu Tehran kwa kukiuka makubaliano ya muda yaliyosainiwa na nchi zote mbili mwezi Juni yaliyolenga kumaliza mzozo huo, akiongeza kuwa βwanadanganyaβ na βwanatapeliβ.
πππππππ
https://youtu.be/VW0oUEaNN4M
2 days ago | [YT] | 0
View 0 replies
Load more