Deutsche Welle ni Shirika la Kimataifa la Utangazaji la Ujerumani, linaloandaa vipindi vya Televisheni, Radio na Mtandao wa Intaneti kwa ajili yako katika lugha 30 - popote ulipo ulimwenguni.

Tafadhali tusaidie kuyafanya majadiliano katika kituo hiki kuwa safi na ya kukubalika na jiepushe kutumia lugha ya kibaguzi au uchafu pamoja na matusi ya kibinafsi.

Kwa taarifa zaidi tafadhali bonyeza link ya "DW Netiquette" hapo chini.
Tunakusihi ushiriki katika utafiti wetu wa mtandaoni ili tupate maoni yako. Bonyeza kiunganishi kwa maelekezo zaidi: surveys.dw.com/c/vcemmsxp
www.dw.com/en/dws-netiquette-policy/a-5300954


DW Kiswahili

Je, unajua kuwa unene uliopitiliza ni miongoni mwa sababu kuu za vifo vinavyoweza kuzuilika? Tatizo hili limekuwa kimya lakini hatari, na linaendelea kuathiri watu wa rika zote. Mjadala huu unalenga kufungua macho yetu kuhusu Obesity, kwa kuelezea chanzo chake, athari zake na namna ya kuchukua hatua mapema. Lakini je unadhani unene uliopitiliza ni kosa la mtu binafsi au ni tatizo linalosababishwa na mfumo wa maisha wa leo? Tuambie maoni yako #dwkiswahili https://www.youtube.com/watch?v=cobH8...

1 month ago | [YT] | 42

DW Kiswahili

Licha ya usitishaji mapigano, shughuli za usafiri zimeripotiwa kuwa ndogo katika Mlango wa Bahari-Hormuz. Marekani imeishutumu Iran kukiuka makubaliano, Tehran nayo ikilaumu mashambulizi ya Israel Lebanon. Rais Donald Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii kwamba Iran yafanya “kazi duni sana” kuruhusu mafuta kupita. Kwingineko, Israel imemkosoa waziri wa ulinzi wa Pakistan kutokana na matamshi yake.Ukosoaji huo umejiri kabla mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika na kati ya Marekani na Iran ambapo Pakistan ndiyo mpatanishi
Kwa mengi zaidi sikiliza matangazo yetu: https://www.youtube.com/watch?v=ddPWZ...
#DWKiswahili #Hormuz #Iran #Marekani #HabariZaUlimwengu #Nishati

1 month ago | [YT] | 17

DW Kiswahili

Wakati usitishaji dhaifu wa vita ukiendelea baada ya zaidi ya mwezi wa mashambulizi ya mabomu, Wairani wana hofu kuwa utawala uliojeruhiwa lakini unaosalia madarakani utawakandamiza zaidi wapinzani wake wa ndani. Kwa mengi zaidi kuhusu taarifa hii, basi bonyeza kiunganisho hiki www.dw.com/en/iran-war-tehran-claims-victory-but-p…

1 month ago | [YT] | 29

DW Kiswahili

Makubaliano ya Iran na Marekani kusitisha mapigano kwa wiki mbili na pia kufungua mlango wa bahari wa Hormuz ila kwa masharti, yamewaacha wachambuzi na maswali ya nani mshindi? Je, wewe mtizamo wako au tathmini yako ni gani?

1 month ago | [YT] | 81

DW Kiswahili

Trump atangaza kusitisha mapigano kwa wiki mbili nchini Iran +++ Zaidi ya watu 180 wafariki au hawajulikani waliko baada ya meli kuzama mediterrania +++ Korea Kaskazini yaendelea kurusha makombora baharini +++ Bayern Munich yaitandika Real Madrid nyumbani.+++ Kwa mengi zaidi basi bonyeza kiunganishi hiki https://www.youtube.com/watch?v=Htq9E...

1 month ago | [YT] | 23

DW Kiswahili

Maisha baada ya mauaji ya kimbari Rwanda: https://youtu.be/5FVuUrseWZQ?si=1_HJv...

1 month ago | [YT] | 4

DW Kiswahili

Watu 13 wamefariki na wengine 57 kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa uliosababishwa na moto katika kambi ya kijeshi nchini Burundi. Jeshi limesema moto huo ulizuka usiku katika ghala la kuhifadhia vifaa vya kijeshi na kusababisha milipuko kadhaa baada ya risasi na mabomu kulipuka. Msemaji wa jeshi, Gaspard Baratuza, amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, akisisitiza kuwa hakukuwa na shambulio lolote dhidi ya kambi hiyo. https://www.youtube.com/watch?v=Cgk9y...

1 month ago (edited) | [YT] | 54

DW Kiswahili

Shirika la anga la Marekani, NASA, limeanzisha safari mpya ya kihistoria kuelekea mwezini kwa kurusha chombo cha Artemis II kikiwa na wanaanga wanne. Safari hiyo ni ya kwanza ya binadamu kuuzunguka mwezi ndani ya zaidi ya nusu karne tangu enzi za programu ya Apollo. Roketi kubwa ilirushwa kutoka kituo cha Safari za anga cha Kennedy, huku maelfu ya watu wakishuhudia tukio hilo muhimu. https://www.youtube.com/watch?v=Cgk9y...

1 month ago (edited) | [YT] | 50

DW Kiswahili

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, amesema nchi yake itatathimini upya mahusiano yake na muungano wa kijeshi wa NATO mara tu vita dhidi ya Iran vitakapomalizika. Amekiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba Washington inalazimika kuangalia upya thamani ya NATO kwa nchi yake, akiongeza kwamba uamuzi huo utafanywa na Rais Donald Trump. Kauli hiyo ya Rubio inakuja muda mchache baada ya Trump kutumia mtandao wake wa kijamii kuzikosowa vikali Uingereza na Ufaransa ambazo zimekataa kujiunga na vita dhidi ya Iran, zikisema hazikushauriwa kabla. https://www.youtube.com/watch?v=ziaZ2...

2 months ago | [YT] | 68

DW Kiswahili

Vita vilivvogeuka kuwa vya kikanda bado hakuna dalili zinazoonesha wazi kwamba mzozo huo utamalizika hivi karibuni. Athari za vita hivyo zimeutikisa ulimwengu katika namna isiyopimika, Je, una tafakari au swali katika viti hivyo? Toa mtazamo wako kwa 'Mjadala Wetu' wa leo. https://www.youtube.com/watch?v=ziaZ2...

2 months ago | [YT] | 51